WABUNGE UGANDA WAANZA MAFUNZO YA KUTUMIA IPAD...
0
Vimbwanga vya matumizi ya Tabiti yaani
I pads nchini Uganda vimeendelea kwa wabunge nchini humo ambao sasa
wanahitaji mafunzo ya kutumia Ipad hizo kutokana na wengi wao
kushindwa kuzitrumia kabisa.
Bunge la Uganda limeingilia kati
kupunguza presha za wabunge hao ambao wanahaha kushindwa kuzitumia
Ipad hizo. Wabunge nchini Uganda wameanza kufanyiwa mafunzo na
kitengo na Tenknoljia IT cha Bunge hilo ili kufaya kazi zao kwa
ufasaha kwani taarifa zote watakuwa wakizipata kupitia Ipad hizo.
Wiki Iliyopita wabunge wote wapatao
375 walipewa Ipad hizo ikiwa ni hatua inayofikiriwa kupunguza matumizi makubwa ya karatasi.