WABUNGE WAKENYA NAFASI YA PILII KWA MALIPO YA JUU DUNIANI...
0
Wabunge wa bunge la Kenya wametajwa
kuwa wapili katik aorodha ya wabunge wanaolipwa zaidi duniani,
wakiwapiku wenzao kutoka nchini zilizoendelea zaidi duniani kama
Marekani, Uingereza na Japan.
Utafiti uliofanywa na Mamlaka huru ya
Viwango kwa Mabunge ya Uingereza(IPSA) ikishirikiana na Shirika la
fedha duniani (IMF) umeonesha kuwa wabunge nchini kenya wanalipwa
mara 220 ya pato la taifa la sh. Elfu 84,624. Kwa mt mmoja mmoja kwa
mwaka.
Wanasiasa hawa wanapata mshahara wa Shs
za Kenya Mill 90 za Tanzania huku pato la
taifa la nchi hiyo likiwa chini ukilinganisha na nchi nyingine
tajiri. Hii inaweza kuelezwa kuwa Wanbunge wanalipwa fedha nyingi
sana.
Hata hivyo, wabunge hawa 416, wakiwemo
wabunge wa kawaida 349, na wale wa Senate(bunge la juu) 67, wanapata
asilimia 54% chini ya wenzao wa nchini Nigeriawanaopata jumla ya Shs
Mill. 16.5 za Kenya takriban Dola 189,500
Malipo haya makubwa yameonekana
kuharibu malipo ya wafanyakazi wa seriklai katika ofisi za Umma
ambapo kima cha chini cha Mshahara kwa wafanyakazi ni Shs 85,790. kwa
mwezi.
Riopoti hiyo inaonyesha kuwa, wabunge
wamabunge manne kati ya matano wapo Afrika. Wakiongozwa na Nigeria,
ikifuata Kenya, Ghana, Indonesia na Afrika ya Kusini.
Wabunge wa Uingereza wanapata kiasi cha
Shs Mill. 91 kwa mwaka, wenzao wa marekani wakipata Mill. 15.1. Kwa
marekani hii ni Asilimia 3.7 huku Uingereza ikiwa asilimia 2.7 ya
pato la taifa.