FUATILIA UCHAMBUZI YAKINIFU WA HOTUBA YA RAIS OBAMA HAPA...

0

Akitumia maneno na mifano ya kawaida kabisa, yake ya  Barack Obama hapo jana ametoa hotuba ya mwaka nchini Marekani hotuba ambayo husikilizwa na kutiliwa maanani pengine zaidi ya nyingine. Katika hali ya kutaka kupunguza makali ya propaganda za kiasiasa zinazoendelea kumjeruhi Rais huyu mashuhuri, Bw. Obama ameita mwaka huu kuwa ni mwaka wa Vitendo, ambapo amesema atafanyakazi na wanasheria ikiwa ni sehemu ya kutafuta ahueni ya maisha kwa familia za kipato cha kati na cha chini.

Katika hotuba yake hii iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu, Rais Obama ameahidi kutumia madaraka yake kuongeza mishahara kwa wafanyakazi, kulinda mazingira ya kufanya kazi hasa kwa wanawake na pia kuelekeza rasilimali zaidi kwa elimu hasa ya msingi.

Swala la Afya lazima hutokea katika hotuba za Rais Obama. Hasa ukizingatia umuhimu wa kusukuma agenda yake ya Obamacare, mradi ambao bado haujaonesha mafanikio ya kutosha.

Hotuba hii ya Rais Obama imekuja wakati ambapo kura za kutathmini utendaji wake hazikurudhisha. Hii inaleta hofu kubwa kuwa huenda katika chaguzi za useneta mnamo mwezi wa 11, chama cha Democrat kinaweza kupoteza nafasi nyingi. Hivyo miezi hii michache ni ya Rais Obama kufanya kila awezalo, kuwashawishi wamarekani katika sera za kiuchumi ilikurudisha imani ya wengi iliyotoweka.

Obama ameliambia bunge la Marekani “The congress” wazi kuwa sio lazima wamruhusu afanye kila kitu au sio lazima apitishe agenda zake zote kwao, lakini anaweza pia kufanya yeye mwenyewe.



Kwa upande mwingine Obama alijibiwa hotuba yake hiyo na mwanamama Cathy McMorris ambaye aliuwakilisha upinzani. Japokuwa Republicans hawalipi swala la usawa katika ajenda zao kwa kuwa wote ni mabepari, walionekana kukubaliana na hilo jana.

Hata hivyo, kutangazwa kwa kima cha chini kwa Rais Obama ilikuwa ni mfano tosha wa mipango yake ya kufanya maamuzi bnila kulishirikisha bunge, japo haijulikani Rais Obama ataweza kufanya hivi kwa muda gani

Kima hichi kitapanda kutoka dola 7.25 kwa saa mpaka dola 10 kwa saa.

Ongezeko hili litaathiri sana watoa huduma kama vile wale wa migahwa mn awa vyombo vya usafiri hivyo kufanya pato la mfanyakazi aliyeajiriw akw amwak akufikia Dola 21,000 kutoka dola 15,000

Tumemzoea akitumia maneno na mifano ya kawaida kabisa kuelezea mambo magumu na yanayoamua mustakabali wa nchi ya Marekani na dunia kwa ujumla. Unadhani mtindo huu wa Obama unamfanya atofautian ana wanasiasa wengine duniani? Na je unaonaje wanasiasa wengine wakiiga mfano wake? 

NB:TOA MAONI YAKO 

0 comments: