ON AMAPENZI YALIVYOTIA DOA WASIFU WA RAIS WA UFARANSA HOLLANDE...Kwa kina
0
Francois Hollande , Bi Valerie Trierweiler |
Taarifa ilikuja kama ilivyoo...Rais wa Ufaransa Francois homllande alipoamua kuzunguza kama mwanaume mwingine wa kawaida na kuweka urais wake pembeni. Alitangaza kuisha kwa mahusiano yake ya kimapenzi na aliyekuwa mwenza wake Bi. Valérie Trierweiler.
Tamthilia hii ya aina yake iliyoendelea kwa wiki mbili mfululizo mpaka kusababisha kupata mshituko na msongo wa mawazo kwa mwenza wake huyu Bi. Valérie Trierweiler sasa imefika tamati.
Wakati Rais aliposafiri kuelekea Vatican ambako hakupewa mapokezi aliyostahili, Nyuma Bi Val;erie alikuwa kifungashatayari kwa kwa kusafiri kuelekea India bila kujua kuwa atakaporudi hata reje atena katika ikulu hii tukufu ya Ufaransa.
Mama huyu alikuwa akishiriki kongamano la kupiga vita njaa nchini India kama mke wa Rais yaani First Lady. Bahati Mbaya sana hii ilitokea wakati Rais Hollande anatangaza kutengana na mama huyu, hivyo vyombo vya habari vilisema kuwa Ufaransa iliwakilishwa na mwananchi wa Kawaida. Masikini Bi Valerie....alivuliwa madaraka yake paohapo. Achilia mbali donda alilokuw analo, alichomwa kwa msumari wa moto.
Licha ya mama huyu kutopata sapoti ya kutosha kutoka kwa wananchi wa Ufaransa, alikuwa pia anatishia Uongozi wa Francois Hollande kwani maelewano mabovu kati ayake na mwenza wake yalitishia hata mikutano ya Rais ya kimataifa ambapo mara kwa mara alipoulizwa kuhusu mama huyu alipatwa na kigugumizi. Mahusiano yake na muigizaji Julie Gayet, mwenye umri wa miaka 41, nayo yalitishia kura ya maoni ya Francois kwani wananchi wengi hawakumpa kura hiyo.
Taarifa iliyotolewa upande wa bi Trierweiler inasema Anachohitaji zaidi Bi Triewiler kwa sasa ni maelezo sahihi kuhusiano na utengano wao ili hadhi na heshima yake isishuke kwani ana Taaluma na fani yakudumisha. “she has a career to keep'
Hata hivyo kwa sasa amechukua mapumziko huko Versailles, na atarudi katika nyumba waliokuwawakiishi na Hollande kabla hajawa Rais.
Hollande amewahi kukiri wazi kuwa Bi Triewiller ni Mwanamke wa maisha yake lakini hawezi kuwa nae kwani ni mbinafsi sana.
Hata hivyo kutengana kwao kumechochewa zaidi na taarifa za hollande kuwa na mahusiano mengine na mwanamke takriban mwezi mmoja uliopita.
Hollande amekuwa na mahusinao na wanawake zaidi ya wanne wengine wakiwa na watoto naye, lakini hakuwahi kumuoa hata mmoja wao. Vijana wengi wa sasa wanadai ugumu wa maisha ndiyo unawafanya wachelee kuoa. Unadhani Rasi Francois Hollande nini kinamfanya asioe?