Ona Wachina walichofanyiziwa siku ya Valentines....Hapa
0
Baadhi
ya wapenzi nchini China leo watakosa fursa ya kukaa kiti kimoja
wakati wakuangalia filamu katika Siku ya Wapendanao, kutokana na
kampeni ya kuwatenganisha iliyoanzishwa na mwanaume mmoja asiye na
mpenzi.
Mwanaume
huyo ambaye jina lake halijajulikana amekuwa akinunua tiketi ya kiti
kimoja katika kila viti viwili za jumba kuu la sinema la Shanghai,
ili kuwadhibiti wapenzi wasikae pamoja kampeni ambayo pia iliungwa
mkono na
watu wasio na wenza nao kununua tiketi kwa mtindo huo.
Siku
ya Wapendano nchini China hutumika kwa kuangalia filamu maalum
inayoonyesha historia ya mapenzi katika Mji wa Beijing.
Mwanaume
huyo amesema kitendo hicho alichofanya cha kuwadhibiti wapendano
kukaa pamoja kuangalia filamu hiyo ni mzaha tu na anatarajia
wapendanao watamuelewa.