MARAIS AFRIKA WAVUTANA MUSTAKABALI WA ICC
0
Marais Barani Afrika wanakutana
mwishoni mwa wiki mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kujadili
uhusiano wa bara la Afrika na mahakama ya kimataifa ya jinai ICC.
Mkutano huu maalum umeitishwa baada ya
ICC kukataa ombi la wanachama 54 wa Muungano wa Afrika kurejesha kesi
za Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto nyumbani. Viongozi hao
wanatarajiwa kujadili hoja ya kujiondoa kutoka kwa mahakama hiyo.
Baada ya miezi kadhaa ya kutofautiana
kati ya ICC na AU, viongozi wa Afrika wanakutana katika makao makuu
ya AU katika kile kinachosemekana ni kutafakari upya uhusiano wa bara
hilo na mahakama ya ICC.