MINYOO WATUMIKA KUANDAA DAMU BANDIA
0
MINYOO WA BAHARINI WANAWEZA KUTUMIKA
KUTENGENEZA DAMU BANDIA KWA AJILI YA MAJERUHI WANAOHITAJI AU
WALIOPOTEZA DAMU NYINGI....
Wanasayansi wa nchi ya Romania wamesema
wanaweza kuwa njiani kukamilisha matayarisho ya damu BANDIA lakini
salama na ya kuaminika kwa matumizi ya binadanmu HASA KATIKA kuokoa
maisha ya watu waliopata majeraha na kupoteza damu nyingi....
Watafiti kwa miaka mingi wamekuwa wakijaribu kutengeza chembechembe
nyekundu za damu (HAEMOGLOBIN ) BANDIA itakayoweza kubeba hewa ya
Oxygen mwilini bila mafanikio. Hata hivyo wanasayansi hwa wa Romania
wamedai kuwa vipimo na majaribio walioyafanya kw akutumia
hemerythrin, chembechembe zilizotokana na minyoo wa baharini wanona
dalili ya kufaulu katik aswala hili.
Utafiti huu umezua utata baada ya
kubadilika kwa damu hii pale inapokutana na kemikali nyingine...Hata
hivyo Prof rossi solagidumitresco na Timu yake katika chuo cha
Bandesi Buyahi amesem akuwa damu hii ilipojaribi wakw apanya
haikuleta maafa yoyote.
…..Prof...Damu hii haifungamani sana
na kemikali nyingine kwenye damu...ambazo kemikali hizi huiharibu
haemoglobini ndani ya sekunde..Lakini hii haiharibiki haraka kiasi
hicho...
Damu hii bandia inatengenezwa na maji
na chumvi pamoja na kemikali maalum. Badala ya kuwa nyekundu kama
ilivyo damu ya kawaida hii hutengeza mchanganyiko wa Njano kwa
mbali..Timu hii inaamini kuwa uvumbuzi huu unaweza kuleta mapinduzi
katika tasnia ya afya...Kama wanavyoonesha Protini maalum ya
kusafirisha damu kwa wanyama wasio na uti kama wajulikanao kama
Invertebrates..inawezesha pia kutumika kwa walionao wanajulikana kama
Vertebrates hivyo Panya walitumiwa. Ili kuhakikisha kuwa kemikali hii
ni thabiti na haiwezi kubadilishwa na kemikali zozote au chembechembe
mwilini, inaweza kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika..
Prof:...Kama damu ya binadamu inaweza
kukaa katika friji kwa miezi na baadae kutupwa kwa kuharibika..hii
tunaweza kuiweka kwenye kabati au tukasafiri nayo...na tukiichanganya
na maji safi..tunapata Damu hapohapo...
Watafiti hawa wanaamini kuwa damu hii
inaweza kutuimika kwa wagonjwa wakliopo njiani kuelekea hospitalini
au hata vitani ambapo hospitali haipo karibu...Wanaendelea kufanya
majaribio yao kwa Panya na ndani ya Miaka 2 wataweza kuanza kufanya
majaribio kwa Binadamu....