ONA UNDANI WA MCHEZO MCHAFU WANAOCHEZEWA SYRIA NA "THE BIG ELEPHANTS"

0

Mazungumzo ya Amani kwa nchi ya Syria yameendelea hii leo. Macho na masikio ya dunia yote yameelekezwa kwa mazungumzo ambayo pengine ugumu wa kumalizika kwake unatisha kuliko ule wa Sudan Kusini.
Au huenda ni matamshi ya Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki Moon aliyesema kuwa kazi ngumu inaanza leo. Japo kuwa kumekuwa na mazungumzo mengine jumatano wiki hii.

Pengine ndiyo sababu hata wadadisi wakubwa wa mambo wanasema sio rahisi kwa mazungumzo haya kufikia muafaka. Serikali ya Rais Assad na waasi wametupiana maneno ya chuki wakati wa mazungumzo yaliyopita hali isiyoashiria vyema sana kwa mazungumzo haya licha yakuitwa pembeni kwa pande hizi mbili na kuzungumza na msuluhishi wao ambaye ni muwakilishi wa umoja wa mataifa Bw. Brahmi.

Iwapo kutakuwa na makubaliano kidogo tu, hayo yanatosha kabisa kuweka msingi wa makubaliano mengine huko mbele. Kwani hata mazungumzo haya yasingefanyika kwani tayari pande hizo mbili nchini Syria zilikwisha weka masharti ambayo kidogo Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Ban Ki Moon asababishe kusiwepo kwa mkutano huu kwani alikwishakiuka kwa kutaka pande zote zishiriki mkiano huu muhimu.

Ni kweli kwamba kwenye meza ya mazungumzo hakuna budi kuwepo kwa wahusik awote wa mgogoro huo. Hicho ndicho Bw. Ban Ki Moon alichotaka kukifanya. Kwa bahati Mbaya upande wa upinzani wa nchii Syria ulikataa kabisa kuwemo kwa Iran, katika mazungumzo hayo japo majeshi ya Tehran yaliusaidia sana uongozi wa Assad kubaki madarakani. Lakini inawezekan Bw. Ban KI Moon anacheza ka mchezo hivi....Kwasababu, kama kweli anataka wahusika wote wa ghasia hizi wawepo, Mbona hakuwaalika Hezbollah, sasa kundi hili linatajwa kuwa kundi kubwa la kigaidi duniani, Hata hivyo waziri wa mambo ya nje nchini Syria Walid Al-Muallem alidiriki kumwambia Bw. Ban Kimoon kuwa yeye anakaa New York Marekani...na hawezi kufahamu hata kidogo undani wa Syria wala ugaidi wa Hezebollah...

Ikumbukwe kuwa, katika mkutano wa Geneva 1, Umoja wa Mataifa ulipendekeza kupitishwa kwa serikali ya mpito huko Syria, yaani ya Upinzani...Hapohapo inaonekana kutaka kumualika Iran ambaye ni rafiki wa serikali iliyopo madarakani kwa sasa...Lakini Kama kweli walitakiwa kuwepo watu wote wanahusika na mgogoro huu utashangaani wakimbizi wangapi au wale waliopoteza makazi yao ndanio ya nchi yaani Internally Displaces persons (IDP) na wamekuw awakimbizi katika nchi za Lebanon, Turkey, Iraq au Jordan.

Nani anawawakilisha hawa? Kwa kuwepo kwa hawa katika meza ya mazungumzo sio tu wataleta umakini wa kufanya jitihada za kutafuta suluhu, bali Ban Ki Moon na wenzie wataona umuhimu wa kumaliza mapiganoharaka, zaidi ya kuleta Propaganda zisizoeleweka. 
 
Haya yote yametokana Raios Bashar Assad anayekataa kung'oka madarakani kwa hiari yake mwenyewe kusababisha vifo vya watu zaidi ya 110,000 na wengine maelfu kuumizwa na kupewa vilema vya maisha....

Ivi Unamuelewa kiongozi anayeng'ang'ania madaraka kiasi hiki?
Tafadhali toa maoni yako.

0 comments: