Ona Vanessa Mdee Alichosema kuhusu Val's d....
0
Vanessa
Mdee, msanii wa muziki ambaye nyota yake inang'ara vizuri kabisa hapa
Bongo, amesema kuwa katika siku hii ya Wapendanao, Valentine wake ni
mashabiki wake wote wa karibu ambao amekuwa karibu nao na kuonyeshana
nao upendo hususan kupitia njia ya mitandao ya kijamii.
Msanii
huyu amesema kuwa, anawapenda sana mashabiki wake kama ambavyo
anaamini kuwa wanampenda pia, na katika ujumbe wake wa siku hii
amewataka kuendeleza upendo kila siku.